Jumatano , 18th Feb , 2026

Kylian Mbappe amegeuka shahidi baada ya hapo jana mchezaji mwenzake Vini Jr kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na mchezaji wa Benfica Gianluca Predtian katima mchezo wa mtoano “Play-off” ya UEFA CL amefunguka akisema;

Kylian Mbappe

"Vinicius alifunga bao la kushangaza akaenda kushangilia, mashabiki wakamzomea, Hilo ni jambo linalotokea katika soka, Baada ya hapo, kukatokea mvutano na wachezaji wa Benfica”

"Baada ya hapo, nambari 25 wa Benfica - sitaki kutaja jina lake kwa sababu hastahili - anaanza kuzungumza vibaya”

"Aliweka shati lake hapa kusema Vinicius ni “Nyani” mara tano, Nilisikia, kuna wachezaji wa Benfica waliosikia pia, baada ya hapo, kila kitu ulichokiona kilianza." - Mbappe