
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa aliyekaa
Mgandilwa ametoa wito huo kwenye ukurasa wake wa facebook alipokuwa akiandika ujumbe kuwakaribisha wakina mama wafanya biashara wa Kariakoo, ambao walitembea wilayani humo kuangalia fursa za biashara na kutafuta maeneo ya uwekezaji.
Kwenye Taarifa hiyo Mgandilwa amesema Kigamboni ndiyo wilaya pekee iliyopo karibu na katikati ya jiji ambapo unaweza kupata eneo la kutosha kwa ajili ya uwekezaji wa aina yoyote ikiwemo maeneo makubwa ambayo yametengwa kwa ajili ya viwanda.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa tayari kina mama hao wameshapewa eneo la kufanyia uwekezaji wao, wakipewa hekari 25 za ardhi.
