Jumatano , 4th Mei , 2016

Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kusimamia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuanza kuvunja vikundi vya ulinzi na usalama katika vyama vyao ili kuliachia jeshi la polisi pekee kufanya kazi hiyo.

Akiongea katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa chama cha siasa cha NRA Tanzania bara Bwana Almas Kisabya amesema, kuachia vyama vya siasa kuwa na vikosi vya ulinzi kwa vigezo vya kulinda mali zao suala ambalo linaweza kufanywa na vyama vingine pia kwa kigezo cha kulinda mali zao ni hatari kwa usalama wa Taifa.

Almasi pia amevitaka vyama kutekeleza maazimio waliokubaliana kwenye baraza la vyama kuusiana na suala hilo nakusisitiza kuwa kifungu cha 11 cha sheria ya vyama vya siasa, sura 258 vyama vya siasa vinapewa haki ya ulinzi wa jeshi la polisi hivyo kuwa na vikundi nikinyume cha katiba ya nchini ibara ya 147.

Aidha, bwana Almasi amekemea malalamiko yanayoelekezwa kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuusiana na migogoro iliyopo kwenye vyama kuwa ofisi hiyo haiegemei upande wowote bali ni ngumu kwa pande mbili zinazolumbana kukubaliana na uamuzi unaotolewa na ofisi ya msajili.

“Lengo si kuingilia mgogoro wa vyama vingine, ila kama kijana mpenda amani ila shutuma zinazoelekezwa kwa mlezi wetu sio njema kwa historia ya siasa za Tanzania” amesema Almasi.