Jumatatu , 16th Jul , 2018

Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu amejikuta kwenye majibizano na baadhi ya wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii wa twita mapema leo baada ya kuambiwa arudishe twiga (Bila kufafanuliwa ni twiga yupi).

Waziri Mstaafu wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu

Majibizano hayo yameibuka ikiwa ni masaa machache baada Mh. Nyalandu kuweka maneno yakutia ujasiri, na ya ushauri wa kutokata tamaa na baada ya maoni akafikia hatua ya kumjibu mfuasi mmoja kwa kumfananisha na watu waliolaaniwa.

Mfuasi huyo aliyekwenda kwa jina la 'Tamankila1' katika mtandao wa Twitta alimwambia Nyalandu kwamba anapaswa kurudisha Twiga ili aweze kueleweka, huku mfuasi mwingine akimwambia kwamba neno moja kwenye biblia ndilo litakalomuokoa ambalo ni lile la "Mimi sikuja kwa wenye haki bali kwa waovu".

"Tamankila1 watu kama wewe wamelaaniwa. Huwezi kuanza siku kwa kusema uongo ili ujisikie umesomeka kwenye mitandao ya kijamii. Ni twiga yupi unayetaka nimrudishe, na nilimchukua wapi. Imeandikwa, waongo wote, sehemu yao ni katika ziwa liwakalo kwa kiberiti" Ujumbe wa Nyalandu kwa mmoja wa wafuasi wake..

Majibizano hayo ambayo bado yameendelea kwenye ukurasa wa Twitta yalitokana na ujumbe ambao Mh. Nyalandu yanayosema "Ukweli katika maisha ni huu, kwamba Mungu hakuachi. Amini katika uwezo na ukuu wake. Ujapopita katika changamoto zozote katika maisha, hata wale wa karibu nawe wakikuacha, Yeye ni Amini na Kweli, hatakuacha, atakupigania, na atakufanya heri kwa ajili ya utukufu wake" Ujumbe wa Nyalandu kupitia Twita.

Tangu alipojiuzulu nafasi ya ubunge wa Singida Kaskazini, Oktoba 30, 2017,  Mh. Nyalandu amekuwa akiandamwa na skendo za kuuza vitalu pamoja na twiga ambapo aliweka wazi kuwa yupo tayari kujibu tuhuma hizo kwa kuwa anajiamini aliitumikia wizara hiyo kwa uaminifu mwaka 2014 - 2015.

Baada ya tuhuma hizo akiwa nje ya uongozi, Nyalandu aliwahi kumjibu Waziri wa Maliasili na utalii wa sasa Dk. Hamisi Kigwangalla kwamba anasikitika sana kuona Waziri huyo akitumia muda wake ndani ya Bunge kumchafua na kumdhihaki ilihali alifanya mambo makubwa ndani ya wizara hiyo ikiwa kupambana na ujangili kwa kiasi kikubwa.

Ujumbe wa Nyalandu uliozua majibizano mtandaoni