
Moja ya nyumba zilizoteketea kwa moto
Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Rufiji wamefika kwenye tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo Agosti 30, 2021.
Nyumba hizo zimeteketea mara baada ya mwananchi mmoja akiwa anasafisha eneo lake moto ulimshinda na kuteketeza nyumba pamoja na mali na thamani zilizopo ndani ya nyumba hizo na hakuna majeruhi yoyote katika ajali hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge (wa kwanza kushoto)
Aidha Aboubakar Kunenge ametoa pole kwa serikali ya wilaya pamoja na wananchi waliokutwa na madhira hayo na kuwapongeza wakazi wa maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi wananchi wenzao huku akiwaagiza uongozi wa wilaya hiyo kufanya haraka kujua tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo.