Jumatatu , 7th Sep , 2015

Mgombea urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amesema kila mtanzania ajipe mwenye ili aweze kwenda kupiga kura oktoba 25 na kuichagua serikali ya ukawa kwa kuwa imepania kuwaboresha maisha.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia na kunadi sera zake kwa wananchi

Akizungumza katia mkutano wa hadhara Mkoani Tabora katiia viwanja vya Polsis Nzega, Mh. Lowassa amesema Serikali kutoka chama cha TANU na CCM, vyote vimeshindwa kuwealetea maendeleo wananchi hivyo hakuna haja ya kuendelea navyo.

Mh. Lowassa amesema bado siku 49 watanzania kuamua kama kuendelea kuishi bila Elimu bora, kuishi bila Maji, kula, mlo moja au miwili au mitatu hivyo Watanzania wanatakiwa kufanya maamuzi katika sanduku la kura.

Kwa upande wake waziri mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye amesema kama Lowassa atafanikiwa kuingia madarakani watanzania walificha fedha nje watazirudisha.