Jumatatu , 16th Sep , 2019

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole - Sendeka ametengua katazo la Halmashauri ya mji wa Njombe, lililopiga marufuku mabasi ya abiria, kushusha katikati ya mji kwa madai ya kwamba katazo hilo linawaumiza wananchi wa hali ya chini.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole - Sendeka

Uzinduzi wa Kituo kipya cha mabasi ulifanyika Mei 11, 2019, ambapo Halmashauri ya mji wa Njombe ilipiga marufuku mabasi ya abiria yaendayo mikoani na vijijini kushusha abiria katika vituo vilivyopo katikati ya mji jambo ambalo limesababisha kuibuka kwa malalamiko mengi kwa wananchi, kwasababu ya umbali wa kituo kipya cha mabasi.

Akitengua marufuku hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha zamani cha mabasi, Olsendeka amesema, maamuzi hayo ameyafanya baada ya kuona wananachi wanatumia fedha nyingi  kukodi tax na pikipiki maarufu kama bodaboda hali ambayo  imesababisha kujenga chuki kati ya serikali na wananchi.

Halmashauri hiyo ilianza kutumia kituo kipya cha mabasi kilichojengwa kwa ufahadhili wa benki ya dunia na uligharimu zaidi shilingi Bil. 9.

Katika hatua nyingine Ole sendeka amesema kuwa, ili kuwapunguzia changamoto ya usafiri atatengeneza kwa gharama zake kituo kidogo cha kushusha abiria jirani na hospitali ya mji wa Njombe Kibena ili magari ya abiria yawe na uwezo wa kushusha abiria, wanapoenda hospitalini hapo kupata matibabu.

Zaidi Tazama Video hapo chini