
Meneja kituo kikuu cha utabiri cha Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Samwel Mbuya
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 10, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio na kusema kwamba hali hiyo hupelekea Jua kuupiga uso wa dunia na ndiyo maana watu wanapata jua la utosi.
"Kinachotokea sasa kuna wakati miale ya jua inatufikia katika uelekeo wa wima moja kwa moja na tunapata vipindi vya jua la utosi, mionzi mingi ya jua inafika kwenye uso wa dunia na kutengeneza joto baada ya kukutana na ardhi," amesema Mbuya.