Penzi la Msodoki chali

Alhamisi , 22nd Feb , 2018

Msanii wa  Hip hop bongo Young Killer Msodoki amekiru kugombana na mpenzi wake Halimaty Msodoki 'Miss Hip Hop' kwa madai kwamba hivyo ni vitu ambavyo haviwezi kuzuilika hasa watu wanapokuwepo kwenye mahusiano.

Msodoki ambaye amedumu kwenye mahusiano na mpenzi wake huyo tangu alipoanza kujulikana kwenye game ya Bongo Fleva ambapo watu wengi walikuwa wakisubiri ndoa amesema kwamba kutengana kwao hakujasababishwa na mapenzi bali mambo mengine ya kawaida kabisa.

Aidha amekiri mbele ya Kamera za eNEWZ  kwamba kwa sasa mrembo 'Miss Hip Hop' amerudi Mwanza kwa mambo yake binafsi lakini pia jamii inapaswa kutambua kwamba maswala ya mahusiano huwa yana mambo mengi ikiwemo ugomvi.

Pamoja na kubanwa kuhusu mwanadada aliyeonekana nyumbani kwake, Msodoki amefunguka kwamba mashabiki zake wanapaswa  kuelewa na kuamini kile wanachokiona kwani hawezi kuelezea maswala mengi kwa kuwa hata yeye anajaribu katika maswala ya mahusiano yakifanikiwa sawa na endapo yakishindikana itakuwa ndio basi. 

Mbali na hayo Rapa huyo kutoka Mwanza amesema watu ambao wanasema na kutabiri kwamba Young  Killer hataweza kutengeneza tena  nyimbo kubwa kama Dear Gambe na alipofikia ndiyo mwisho wake na kusema kwamba watu wanaobet kwenye mziki wake ni sawa na kutema mate kulia na kufukia kushoto.