Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu amesema zao la korosho ambalo awali soko lake halikwenda vizuri kutokana na utaratibu uliokuwa ukitumiwa na wafanyabiashara kwa kutenga bei ndogo na wakulima wenyewe kugomea bei hiyo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo, Januari 27, 2019) wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho Mtwara, lengo likiwa ni kupata taarifa juu ya mwenendo mzima wa zao hilo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa, taarifa iliyotolewa na timu ya uhakiki ilisema msimu wa 2018/2019 matarajia yalikuwa ni kuvuna tani 150,000 kutokana na kushuka kwa uzalishali.
“Lakini kwa kazi nzuri iliyofanywa na timu nzima ya Wizara, wilaya na mkoa na timu ya uhakiki hadi sasa korosho tulizozipokea ambazo ziko katika maghala ni zaidi ya tani laki mbili.”

