
Tukio hilo limetokea Desemba 17 mwaka huu majira ya saa 2 kamili usiku, hii ni baada ya mtoto huyo kufungwa nguo mwilini mwake kisha kutupwa bila msaada wa aina yoyote.
Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza, liemeendeleza kumtafuta aliyehusika katika kutenda tukio hilo ili aweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, kujibu madai hayo.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema, "tunawaomba wananchi pindi wanapomwona jirani ni mjamzito alafu baada ya muda ghafla ujauzito wake unapotea na mtoto haonekani watoe taarifa polisi ili tuweze kujiridhisha juu ya usalama wa mtoto."