Jumatano , 27th Apr , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa kuelekea uzinduzi wa filamu maalum ya The Royal Tour Tanzania, limejipanga vyema kuhakikisha dunia inashuhudia uzinduzi huo utakaofanyika kesho Aprili 28, 2022,  mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, ACP Justine Masejo

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, amewaambia wananchi kuwa hali ya ulinzi na usalama katika jiji hilo ni shwari kuelekea uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour.

Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionesha Dunia ukarimu huo na kwamba Arusha ni kitovu cha utalii.