Polisi wazuia Mkutano wa Zitto Kabwe, waeleza

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limezuia mkutano wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kwa kile ilichokisema ni sababu za kiusalama. 

Mbunge Zitto Kabwe akifanya Mkutano.

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika Viwanja vya Mwanga Center Mjini Kigoma leo Januari 17, 2020.

Kwa mujibu wa barua ambayo amekabidhiwa Katibu wa Mbunge huyo ambayo imesainiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kigoma Raphael Mayunga amesema wameamua kuzuia mkutano huo kutokana na sababu za kiusalama.