Alhamisi , 4th Aug , 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa anesena kuwa serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mfanyakazi yoyote wa Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia, (TAZARA), atakaejihusisha na vitendo vya kuihujumu mamlaka hiyo.

Profesa Makame Mbarawa akiongea na Viongozi pamoja na Wafanyakazi wa TAZARA

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya wakati akizungumza na wafanyakazi wa Tazara mara baada ya kukagua maeneo mbalimbali ya karakana ya Mbeya inayotoa huduma ya matengenezo ya vichwa vya treni za Tazara.

Mhe Mbarawa amesema kuwa watumishi ambao huwa wanaagiza vifaa vya mawasiliano na matengenezo lakini matokeo yake vinaletwa vifaa hafifu na wakati mwingine haviwasilishwi na kujinufaisha wao wenyewe kutokana na fedha za vifaa hivyo.

Prof. Mbarawa amesema kuwa zoezi hilo halitachagua nchi iwe aliebainika kufanya hivyo awe ni mtumishi kutoka Tanzania au Zambia hatua kali dhidi yake zitafuata ili kukomesha kabisa matukio hayo yanayopelekea shirika hilo kuyumba kiutendaji.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa ubinifu ili kuibua mbinu mpya za kibiashara na kulifanya shirika hilo kuwa chachu ya Maendeleo kwa nchi zote mbili.