Jumatano , 2nd Nov , 2022

Rais Samia Suluhu, amesaini sheria ya marekebisho ya usimamizi wa rasilimali za maji ya mwaka 2022 (The Water Resources Management Act, 2022) kitendo ambacho kinatajwa kuimarisha bodi za mabonde ya maji katika kusimamia rasilimali za maji vilevile kuimarisha uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa na Rais Samia Suluhu Hassan

ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji majumbani na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni Dodoma Dkt. Tulia Ackson jana Novemba Mosi 2022.

Wadau mbalimbali wamempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kutambua umuhimu wa utunzaji, uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za maji wakieleza kwamba Muswada huo umekuja wakati sahihi ambapo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya maji ikiwa kiwango cha rasilimali za maji kiko palepale.

Aidha, Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema;
"Hii ni taarifa njema kwetu na ni alama kubwa katika sekta ya maji katika eneo hili muhimu la rasilimali za maji ikiwa kwa kuelekea kwenye mageuzi ya kweli katika mustakhabali wa usimamizi wa utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji ambayo ndio roho ya upatikanaji wa maji, kwa dhati kabisa Wizara ya Maji tunamshukuru Mhe Rais kwa kuandika historia hii,".

Ikumbukwe Septemba 15, 2022, Bunge lilipitisha Muswada huu wa Sheria ya Marekebisho ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2022.