Alhamisi , 20th Oct , 2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein  Mwinyi leo Oktoba 20, 2022 amemteua Is-haka Khamis kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi, Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Said imesema kuwa kabla ya uteuzi huo Is-haka alikuwa Naibu Mwenyekiti wa Mahakama  ya Ardhi, Unguja .

Uteuzi huo umeanza leo Oktoba 20, 2022