Jumanne , 26th Mei , 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaaga rasmi mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi katika mkutano wa siku nne ulioanza leo jijini DSM.

Katika salam zake Rais Kikwete amewataka wawakilishi hao wa nchi kuhakikisha kuwa wanaendeleza diplomasia nzuri ya kimataifa iliyojijengea Tanzania ambayo mara zote imehakikisha kuwa inakuwa na maadui wachache na marafiki wengi.

Rais Kikwete amewataka mabalozi hao kuacha kukaa maofisini na badala yake watumie fursa waliyopewa kutafuta fursa zitakazosaidia nchi kuendelea kiuchumi.

Kwa mujibu wa rais Kikwete, Tanzania imefanikiwa kujijengea heshima kimataifa, heshima ambayo haiendani na uwezo wa nchi kiuchumi na hivyo kuna haja ya mabalozi hao kubadili mtazamo wa namna wanavyofanya kazi kwa kuhakikisha sifa hizo zinaendana na uwezo kiuchumi pamoja na masuala ya ulinzi.

Mkutano huo pia unalenga kuangalia fursa za diplomasia ya kimataifa katika kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025;