Ijumaa , 11th Apr , 2014

Rais  Dkt Jakaya Mrisho  Kikwete  ameongoza  jopo  la  viongozi  wakiwemo  marais  wastaafu   katika  maadhimisho  ya  kumbukumbu  ya  miaka  30 kifo  cha aliyekuwa  waziri  mkuu  wa  Tanzania  hayati  Edward  Moringe  Sokoine.

Kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Hayati Edward Moringe Sokoine.

Rais  Dkt Jakaya Mrisho  Kikwete  ameongoza  jopo  la  viongozi  wakiwemo  marais  wastaafu   katika  maadhimisho  ya  kumbukumbu  ya  miaka  30 kifo  cha aliyekuwa  waziri  mkuu  wa  Tanzania  hayati  Edward  Moringe  Sokoine  yatakayofanyika  wilayani  Monduli mkoani  Arusha.
 
Mkuu  wa  mkoa  wa  Arusha  Magesa  Mulongo  ndiye aliyekuwa mwenyeji wa ugeni uliohudhuria maadhimisho  hayo  yaliyoshirikisha  baadhi  ya  viongozi  walioshiriki  ni pamoja  na  Rais  wa  awamu  ya tatu Benjamini Mkapa, mjane  wa  baba  wa taifa  mama  Maria  Nyerere, watendaji mbali mbali wa  serikali na  wananchi kwa ujumla.
 
Katika maadhimisho   hayo  shughuli  mbalimbali  zimefanyika  kwa  lengo  la  kumuenzi  kiongozi huyo  shujaa  aliyepigania  wanyonge  katika  kipindi chote  cha  maisha  yake na  kwamba  makundi  mbalimbali  yamejitokeza  kushiriki  kufikisha  ujumbe  unaolenga kuenzi na kuendeleza yote aliyaanzisha  hayati  Edward  Moringe Sokoine aliyefariki  mwaka  1984  kwa  ajali   ya gari.

Rais Kikwete amesema Serikali itaendelea kuyaenzi yote ambayo Hayati Sokoine aliyapigania ikiwa ni pamoja na uadilifu pamoja vita dhidi ya rushwa.
 
Baadhi ya wananchi maeneo mbalimbali ya mkoa  wa  Arusha wameyaelezea  madhimisho hayo  kwa  mitazamo tofauti  sambamba na  kutoa  maoni  yao jinsi  watanzania  wanavyoweza  kumuenzi  kiongozi  huyo.
 
Maadhimisho hayo yamefanyika  nyumbani  kwa  familia  ya  hayati  Sokoine  kata ya Monduli juu Wilayani Monduli.