Jumatano , 6th Dec , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatano Disemba 6 amefanya uteuzi wa Wenyeviti 6 wa bodi za taasisi za Serikali baada ya waliokuwepo kumaliza muda wao.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jioni ya leo imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Bi. Monica Ngezi Mbega kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuanzia Novemba 30, 2017.

Wengine walioteuliwa ni kama wanavyoonekana kwenye taarifa hiyo hapo chini ambayo ina majina yao pamoja na bodi wanazokwenda kuzitumikia.