
Bashungwa ametoa kauli hiyo leo Bungeni Dodoma ambapo amesema kuwa zipo taasisi ambazo zinazua taharuki kwa watanzania bila sababu za msingi
"Unakuta mtu hajasajili kanisa, anatoa huduma, anaamka anasema ameomba ameoteshwa kwamba sijui kitatokea nini. Kama umeona umeoteshwa kutakuwa kuna hali ambayo siyo nzuri, basi nenda uombe Mwenyezimungu aizuie isitokee kwenye taifa letu, lakini siyo kutoa taharuki kwa taifa kwamba jana nimelala, nimeota, mimi ni nabii, kutakuwa na taharuki hii"
"Sasa mimi nilitegemea huyohuyo kiongozi angeenda amuombe Mwenyezimungu, aombe hilo balaa lisitokee, lakini kiongozi huyo analeta taharuki ya nchi, Watanzania waache kufanya shughuli zao waanze kupaniki, lakini ukifuatilia unakuta hajasajiliwa, ukimgusa anasema serikali inavamia viongozi wa dini, kwahiyo tunakwenda kufanya uchambuzi vizuri, tutaleta mbele ya bunge hili, tuwaoneshe wale ambao wanafanya kazi kinyume cha utaratibu ili tutakapowachukulia hatua, Watanzania wajue kuwa siyo mambo ya kisiasa" - amesema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Innocent Bashungwa bungeni leo Jumanne Juni 3, 2025.