Rais Magufuli atoa ndege zake kwa wananchi

Ijumaa , 11th Jan , 2019

Rais Dkt. Magufuli ameagiza kwamba ndege 2 kati ya ndege 3 za Rais, zipakwe rangi ya Air Tanzania na zianze kutumika kusafirisha abiria.

Rais Magufuli akishuka kwenye ndege ya Rais katika moja ya safari zake.

Ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 11, 2019 wakati wa mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

''Badala ya ndege hizo kukaa bila kutumika ni bora zitumiwe kusafirisha abiria kwenda sehemu mbalimbali ili kuhakikisha wigo wa kukuza utalii unaongezeka'', amesema.

Aidha Rais Magufuli ameshwashukuru wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwa kuwezesha maendelo hayo kupitia kuunga kwao mkono bajeti inapopelekwa bungeni.

Airbus 220-300 imekuwa ni ndege ya 6 kuwasili nchini miongoni mwa 7 zilizonunuliwa na Serikali huku nyingine moja ikisubiriwa ambapo leo Rais amethibitisha kuwa ndege nyingine ya 8 inanunuliwa.