Jumatano , 16th Dec , 2015

Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk. Edward Hoseah,

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk. Edward Hoseah, kutokana na kutoridhishwa namna taasisi hiyo inavyotekeleza wajibu katika kupambana na rushwa hususan katika upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue amesema kutokana na kutenguliwa uteuzi huo Rais Dk. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa TAKUKURU.

Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema rais Dk. Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja watumishi wanne waandamizi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambao walisafiri nje ya nchi licha ya rais kupiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watumishi wa umma.