Jumatano , 14th Dec , 2022

Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt Hashil Abdallah kuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara . Kabla ya uteuzi huo Dkt Abdallah alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa hii leo Desemba 14, 2022, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus, na kwamba uteuzi wa viongozi huo umeanza rasmi Desemba 9 mwaka huu.

Aidha Rais Samia amemteua Kaspar Mmuya, kuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Mumuya alikuwa ni Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).