Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, tayari amekwishawasili nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye,

Rais Ndayishimiye amewasili mapema leo asubuhi ya Oktoba 22, 2021, jijini Dodoma, kwa ajili ya ziara yake ya kitaifa ya siku tatu ambapo pia atapata fursa ya kwenda Zanzibar na kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Hussein Mwinyi.

Pamoja na mambo mengine pia Rais Ndayishimiye anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha mbolea, kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukagua ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaoendelea nchini kutokea stesheni ya Dar es Salaam hadi stesheni ya Kwala - Ruvu pamoja na kutembelea bandari kavu ya Kwala inayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika eneo hilo.