Jumatano , 7th Dec , 2022

Dkt Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa kachaguliwa kwa kura za ndio 1914 kati ya kura 1915 na kura 1 imesema hapana. 

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM

Rais Samia amechaguliwa hii leo Desemba 7, 2022, na Wajumbe wa chama hicho katika mkutano mkuu wa 10 wa CCM uliofanyika Jijini Dodoma.

Aidha Wajumbe wa CCM pia wamemchagua Abdulrahman Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi kingine tena. Kinana amechaguliwa kwa kura za ndiyo 1913.

Ambapo pia Dkt.Hussein Ally Mwinyi amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kupata kura za ndiyo 1912 kati ya kura 1915 na kura 3 zimesema hapana.