Ijumaa , 10th Sep , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya serikali kununua mahindi yote ya wakulima ili kuwasaidia kuondokana na adha ya utafutaji wa masoko ya mazao yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 10, 2021, Bungeni Dodoma, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo amesema kuwa shughuli za ununuaji wa mahindi hayo zitaanza Jumatatu ya Septemba 13 mwaka huu.

Tazama video hapa