
Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia ametengua uteuzi huo wa Kamishna Diwani Athumani Msuya ambaye Januari 3/2023 aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Dkt. Samia amemteua Bw. Mululi Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Bw. Mahendeka kabla ya uteuzi wake alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Ikulu