
Rais wa Brazili Bi Rousseff
Uamuzi uliofikiwa na Bunge hilo ni kumsimamisha kazi ya urais kwa siku 180 wakati bunge hilo la Seneti likiendelea na uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Bi Rousseff anatuhumiwa kutumia kinyume cha sheria fedha za serikali katika uchaguzi wa mwaka 2014 , hivyo Makamu wa Rais Michel Temer sasa ndio atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.
Rousseff alichukua hatua ya mwisho kujiokoa kwa kukataa rufaa katika mahakama ya juu zaidi nchini humo kusitisha kura hiyo, lakini hatua hiyo ilipingwa.