Hii itakuwa ziara ya pili ya Zelenskyy nchini Poland baada kuitembelea nchi hiyo mnamo mwezi Disemba katika safari iliyompeleka pia Marekani.
Miongoni mwa mambo atakayoyafanya Zelenskyy katika ziara hiyo ni pamoja na kuzungumza na raia wa Ukraine waliopewa hifadhi ya ukimbizi nchini Poland.
Ziara ya Zelenskyy inafanyika siku kadhaa baada ya Ukraine kutangaza mipango ya kununua magari 100 ya kivita kutoka Poland kupitia ufadhili utakaotolewa na Marekani na Umoja wa Ulaya.





.jpg?itok=5cvL0YaP)