Ijumaa , 3rd Jun , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametoa siku 14 kwa wananchi zaidi ya 700 wa Mtaa wa Mbondole Wilaya ya Ilala waliovamia na kujenga kwenye eneo la Mzee Martin Nasson kuondoka na kutoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla

RC Makalla ametangaza maamuzi hayo Baada ya Kukosekana kwa muafaka baina ya Mmiliki aliyepewa haki na Mahakama kushindwa kukubali ombi la Wavamizi waliotaka kumlipa fidia ili waachwe kwenye eneo Hilo.

Kutona na Hilo RC Makalla amesema ifikapo tarehe 18 mwezi huu asionekane mtu kwenye eneo hilo na kusisitiza kuwa siku 14 zilizotolewa ni Huruma ya Serikali kwakuwa tayari walishaamuriwa na Mahakama kuondoka tokea muda mrefu.

Hata hivyo RC Makalla amesema Serikali itaendelea kuheshimu maamuzi yanayotolewa na Muhimili wa Mahakama katika kusimamia Sheria.

Pamoja na hayo RC Makalla amewatahadharisha Wananchi kuacha tabia ya kuvamia au kununua maeneo pasipo kujiridhisha na Nyaraka za umiliki