Akizungumza na www.eatv.tv, Adam Malima amesema kwamba pesa hizo ndio kitu cha muhimu kwake kwa sasa, kwani zinatakiwa kwenda kufanya shughuli za maendeleo, na sio kumletea majibu ya kisiasa yasiyo na faida.
Akiendelea kuzungumzia hilo Adam Malima amesema kwamba amewaambia madiwani wote mkoani humo kumpa majibu haraka iwezekanavyo, na kutoa siku tatu za kufanya hivyo.
“Nikamwambia DC mpya kwamba wewe umekimbiza mwenge ulikuwa unakataa miradi kwa kupungukiwa milioni moja tu, sasa tunataka kujua bilioni 9.5 ziko wapi, nimewaambia madiwani wa CCM na CHADEMA, nawapa siku tatu, Jumanne au Jumatano niende waniambie wao kama madiwani, kwa nini wana uhalali wa kuwa madiwani kama hawawezi kujua hizi pesa ziko wapi, kwa sababu zinatakiwa kutumika kwa shughuli za maendeleo”, amesema Adam Malima.
“Watu wanahangaika na hawana majibu kwenye hiyo pesa, nataka kupata hizi pesa, nijenge madarasa, zilete huduma bora za afya, na miradi ya maji, sasa nataka kujua where is my money, ukiniambia pesa hii imekwenda hivi sawa, unatengenza uongo kuwa umewapa makundi ya kina mama, show me the money”, amesisitiza RC huyo wa mkoa wa Mara.
Kufuatia huo kuliibuka sakata lingine la kumuweka ndani mmoja wa madiwani wake kwa kosa lililotajwa kuwa 'alikunja nne', na kusema kwamba hakumuweka ndani mtu huyo, isipokuwa alimtoa mkutanoni kwani hawezi kuvumilia vitendo vya utovu wa nidhamu, alivyokuwa akivifanya mbele yake.
“Sasa upuuzi wa huyo Bwana, mimi mwenyewe nakaa kwenye mkutano naweka nne, lakini 'don't dis respect the meeting', hata yeye mwenyewe anajua, mimi nimemtoa nikaenda zangu kuresolve mgogoro wa vijiji, baadaye nikasikia yuko ndani, nikasema alaa, kumbe yuko ndani, basi mtoeni”, amesema Adam Malima.





