Jumatatu , 9th Sep , 2019

Taharuki imezuka mkoani Katavi, kufuatia kuibuka kwa tetemeko la ardhi mkoani humo, ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.2 katika vipimo vya Ritcha.

Akizungumza mkoani humo Kamanda wa Polisi mkoani Katavi, Benjamini Kuzaga, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 9:00 usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2019 lakini hakuna madhara yaliyotokea.

"Ni kweli kuna tetemeko la ardhi ambalo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:00 usiku na limedumu kwa dakika 3, lakini mpaka sasa hivi hakuna madhara kwa binadamu wala aliyeathirika kwa tetemeko hilo"

"Wilaya zote za Katavi zimekumbwa na tetemeko hilo, tumezungumza na Wakuu wa Ulinzi na usalama wamesema limetokea, watu bado wanaendelea na shughuli zao na tuaendelea kuwasiliana na wenzetu ili tuone namna ya kulikabili sasa hivi'', ameongeza.

Aidha Kamanda amewataka wakazi wa mkoa huo kukaa maeneo ya wazi, ili waweze kujikinga pindi tetemeko hilo litakapotokea tena.