Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya
Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa hii leo Oktoba Mosi, 2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,
Akizungumza Mahakamani hapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arusha Amalia Mushi, amesema hatua hiyo imekuja kutokana na maandalizi ya maamuzi kutokamiliki.
Katika kesi ya msingi, Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 9 mwaka huu.







