Jumatatu , 15th Apr , 2019

Umoja wa vyama nane vya upinzani nchini umemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kuumaliza mgogoro baina ya Bunge na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini CAG, Prof Mussa Assad kwa kumtaka kukubali kujishusha.

Spika Ndugai

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa Chama cha UPDP, Fahami Dovutwa wakati viongozi hao wakitoa msimamo wa pamoja juu ya masuala mbalimbali yanayotokea nchini.

Dovutwa amesema kuwa, "mambo kama haya madogodogo Spika baada ya kuona ushauri wake hausikilizwi angeshuka tu, ndiyo spiriti ya Watanzania. Viongozi wengi wanapoona jambo lao halisikilizwi huwa wanashuka, nimtake CAG asimame na msimamo wake upinzani tuko pamoja naye."

"Leo amemkataa CAG, kesho akiwa na shauri mahakamani anaweza kuleta hoja ya kumkataa Jaji Mkuu, kesho kutwa atamkataa IGP, mwishowe ataleta hoja ya kumkataa Mkuu wa Majeshi, sasa Taifa litaendaje kwenye masuala kama hayo." ameongeza Dovutwa.

Mgogoro baina ya Spika Ndugai na CAG Prof Assad umedumu kwa muda mrefu hivi sasa kufuatia kauli ya CAG aliyoitoa akiwa nje ya nchi ya kuwa Bunge ni 'dhaifu'.