Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania (Aliyeshika bendera ya Tanzania) tayari kwa matembezi
Mafunzo hayo yatakuwa ni katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning hapa nchini, na kuratibiwa na shirika la AMREF Health Africa Tanzania
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.
Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya afya bure kwa makundi maalum.
Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.
Washiriki