Rais Samia akishuhudia zoezi la utiaji Saini wa mikataba mbalimbali Dubai
Leo Februari 27 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshuhudia zoezi la utiaji saini wa mikataba mbalimbali baina ya Tanzania na wawekezaji, na sekta binafsi na wawekezaji huko Dubai, ikiwa ni matokeo ya maonesho ya Dubai EXPO 2020.
Katika zoezi hilo mawaziri wa Tanzania wametia saini mikataba hiyo ikiwa pamoja na waziri wa Mawasiliano na teknolojia ya Habari Nape Nnauye pamoja na Waziri wa kilino Hussein Bashe
Katika msafara huo Rais Samia pia ameambatana na wafanyabiashara wa Tanzania akiwepo Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji.


