
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja,
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Njelu aliyetaka kujua endapo serikali inaona haja ya kupunguza eneo la hifadhi ya msitu huo kwa wananchi.
Ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa hifadhi hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, ni kulinda vyanzo vya maji vinavyotumika kwa matumizi ya binadamu na wanyamapori.
Aidha, amesema sheria ya msitu huo inaruhusu shughuli za uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo.