Ijumaa , 3rd Jun , 2016

Serikali imesema kuwa itasambaza madaktari bingwa katika mikoa tisa yenye uhaba mkubwa wa madaktari hao ili kuboresha sekta ya Afya katika maeneo hayo na kuepusha gharama za wagonjwa kusafirishwa mbali kwenda kupata huduma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu,

Akiongea leo bungeni Mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, amesema kuwa watatoa kipaumbele kwa madaktari na wahudumu wa afya ambao wapo tayari kufanya kazi mikoani.

Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika Mikoa ambayo itapewea kipaumbele ni ile inayoonekana ina upungufu mkubwa wa watumishi hao ikiwemo Mkoa wa Tabora, Kigoma, Mara, Katavi, Rukwa Simiyu na mingineyo ya Pembezoni.

Waziri Ummy ametumia nafasi hiyo kuwaambia madaktari na wahudumu wa Afya wanaotafuta ajira serikali kuwa hawatua na nafasi kwa Daktari ambae atataka kukaa Dar e s Salaam kwa hiyo watatoa vipaumbele kwa wale ambao wako tayari kwenda pembezoni.

Sauti ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu,