Jumanne , 8th Jul , 2014

Serikali ya Tanzania imesema ipo mbioni kuanza kutoa kipaumbele kwa bidhaa zinazotengenezwa hapa

Waziri wa kazi na ajira Bi. Gaudensia Kabaka.

Serikali ya Tanzania imesema ipo mbioni kuanza kutoa kipaumbele kwa bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini na vijana wabunifu ili kuendelea kuhamasisha vijana kujiajiri kupitia ubunifu wa bidhaa mbalimbali .

Akiongea jijini Dar es Salaam hapo jana Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania Mhe. Gaudensia kabaka amesema kuwa ubunifu wa watanzania umeendelea kuiweka nchi katika sehemu nzuri ya hali ya ajira pamoja na kuongezeka kwa kazi zenye tija.

Waziri Kabaka amesema vijana wengi wameonyesha ubunifu wa hali ya juu huku changamoto kubwa ikiwa ni vifaa vinavyotengenezwa na vijana hao mara baada ya kuhitimu vyuo mbalimbali vya ufundi wanashindwa kuajiriwa hivyo suluhisho pekee ni kujiajiri.