Jumatano , 4th Mei , 2016

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla, amezitaka taasisi za serikali zinazodaiwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), mkoani Mbeya kulipa madeni yao ili shirika hilo liweze kujiendesha na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla

Akizungumza na watumishi wa Tanesco jijini Mbeya Makalla amesema shirika hilo linazidai taasisi za umma na watu binafsi jumla ya shilingi bilioni 7.3 jambo linalopelekea kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kutokana na hali hiyo Makalla amesema atawasiliana na mawaziri wa taasisi husika kuhusu kulipa madeni yao haraka.

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco mkoani Mbeya Injinia, Fransis Maze amemweleza mkuu wa mkoa kwamba taasisi na mashirika ya serikali vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ni miongoni mwa wadaiwa sugu.