Jumamosi , 24th Mar , 2018

Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Magufuli imekanusha taarifa ya kufungia mitandao ya kijamii kama inavyoelezwa na baadhi ya watu na kuitaka jamii kuzipuuza endapo watakutana nazo mitandaoni.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa asubuhi ya leo katika ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema taarifa hizo ni uzushi mtupu hazina ukweli wowote ambayo imetengenezwa na wahalifu wa mtandao.

Leo (Machi 24, 2018) imesambazwa barua iliyokuwa inaonesha kutoka Ikulu ambayo imeandika taarifa za kuwa serikali inawaasa watanzania wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuitumia kwa uangalifu na tija ili kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Soma hapa chini barua yenyewe jinsi ilikuwa imeandikwa