Jumapili , 17th Jan , 2016

Serikali ya Tanzania imeamua kulifungia na kulifuta kutoka katika daftari la usajili wa magazeti, gazeti lugha ya Kiswahili la Mawio ambapo pia hatua hiyo pia inazuia gazeti hilo kuchapishwa katika njia ya mtandao.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza

Akitangaza uamuzi huo Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni Mhe. Nape Nnauye amesema hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa kutokana na mwenendo wa uandishi usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani.

Aidha Mhe. Nape ametoa wito kwa wamiliki,Wahariri,Waandishi na Watangazaji wa habari kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zkizingatiwa hakutakua namigogoro yoyote.

Hata hivyo Nape amesema kuwa serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili,weledi na sheria za nchi na kwamba serikali itaendelea kushirkiana navyo na kutoa ushurikiano kwa wakato wote.