
Akizungumza wakati wa kuchoma shamba hilo mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka amesema oparesheni hiyo maalumu inalengo la kutokomeza kilimo hicho cha bangi pamoja na uhalifu ambao upo hasa uhalifu wa Mifugo ndani ya wilaya hiyo
Nao viongozi wa serikali ya kijiji cha tatwe wanatoa wito kwa wananchi wao kuacha kujishuhulisha na kilimo hicho cha madawa ya kulevya na badala yake wafanye kilimo cha halali ambacho kitawaingizia kipato
Aidha mkuu wa Wilaya amesema wanaendelea.kuwasaka watu wanaojihusisha na kilimo hicho cha bangi pamoja na kuendelea kutokomeza wezi wa mifugo ambao wamekuwa wakiwasumbua wananchi kwa kuwaibia mifugo