
Katibu tawala msaidizi sekta ya uchumi na uzalishaji mkoani Mwanza Emily Kasagala
Kauli hiyo ameitoa wakati akiweka wakfu jengo la bweni la wavulana katika kituo cha kusaidia watoto wenye mahitaji maalum kilichopo eneo la Nyasaka Manispaa ya Ilemela sambasamba na maadhimisho ya miaka 25 ya huduma ya kituo hicho.
" Na kujiepusha na vitendo vibovu vya wizi wa mitihani kama ambavyo tumesikia mwaka huu baadhi ya shule zimefutiwa matokeo kwa sababu ya mashindano kwamba shule yangu iwe bora sasa matokeo yake ni kwamba tunaandaa wataalamu ambao hawana taaluma ya kutosha matokeo yake tunakuwa na madaktari ambao siyo madaktari kamili" amesema Kasagala