'Sitaki mwanaume asiyekuwa na pesa' - Lulu Diva

Jumapili , 8th Sep , 2019

Msanii wa Bongo Fleva Lulu Diva amesema hajawahi kuhongwa, wala kujihusisha na kimapenzi na mtu ajipatike kipato, ila amesema hawezi kuwa na mwanaume ambaye hawezi kumuhudumia.

Lulu Diva ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV cha kila Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana, ambapo amesema tuhuma za kudanga si kweli.

"Kiukweli sijawahi kudanga, ila kuhusu gari ninayoitumia nilipewa na mpenzi wangu wakati wa birthday yangu, kwa hiyo nikipewa na mpenzi wangu siwezi kusema ni kudanga." amesema Lulu Diva

"Mimi sijawahi kudanga, ila siwezi kuwa na mwanaume ambaye hawezi kunihudumia, siwezi kuwa na Mario, mwanaume ambaye hana kazi hata nikimwambia nina tatizo hili, hawezi kunisaidia" amesema Lulu Diva

Kwa sasa Lulu Diva anatamba na ngoma ya Chekecha.

Tazama mahojiano kamili hapo chini.