Jumamosi , 20th Nov , 2021

Baadhi ya maduka ya nguo na magenge ya wajasiriamali wa mboga mboga katika soko la CCM Katoro mkoani Geita yameteketea kwa moto majira ya saa 11:00 alfajiri ya leo Novemba 20, 2021, huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.

Mabaki ya vibanda vilivyoungua kwa moto

Itakumbukwa hii ni mara ya pili tangu maduka manne kwenye soko la wafanyabiashara Katoro kuteketea kwa moto katika soko hilo.

East Africa TV bado inafuatilia tukio hili kwa ukaribu ili kujua hasa ni nini chanzo cha moto huo.