Picha sio halisi
Rehema Mwaluanda ni Bibi aliyekuwa akiishi na mtoto huyo, amesema mtoto huyo alikuwa amelala na wenzake wawili lakini watoto hao wamekuja kushtuka asubuhi mwenzao hayupo, huku milango ikiwa imefunguliwa.
Bibi huyo amedai hajui aliyemtoa mtoto nje na kumuua, kwani haikuwa rahisi kwa mtoto huyo kufungua milango yote, kwani nyumba yake ina milango miwili ya kutokea nje, mmoja wa chuma na mwingine wa mbao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Sonngwe George Kyando, amethibitisha na kusema wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo kama ni visa, kisasi au imani za kishirikina.








