Alhamisi , 12th Sep , 2019

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amemzuia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujibu maswali ya Wabunge wawili Chama Cha Mapinduzi, akiwemo Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jaku Hashim,

kwa kile alichokieleza Wabunge hao walikuwa hawana maswali ya msingi.

Spika Ndugai amefanya maamuzi hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, kwenye muendelezo wa vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Mbunge wa kwanza kuuliza swali kwa Waziri Mkuu alikuwa Mbunge Jaku ambaye alihoji, "katika Tanzania, Zanzibar imo japo hujafika Waziri Mkuu, kwenye Muungano ipo suala la elimu ya juu, majuzi Waziri Ndalichako alishinikiza wanafunzi kwenda China, Zanzibar hatujapata hata mmoja?

Spika : Haya mambo yanayohusu Muungano inahitaji tafiti, kuja na kitu kiko kamili, twende kwenye swali jingine."

Kwa upande wake Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea amehoji "kuna fursa kwa vijana, na kijana anaanzia 18 hadi 35, wengi wao wako masomoni, naomba umri wa ujana utoke 35 hadi 40.

Spika Ndugai : Hii ni sheria na imetaja vijana hoja yako nini?

Mbunge Mtolea : Tukienda kwenye fursa tuwaangalie wanaolengwa kusaidiwa.

Spika Ndugai : Bahati mbaya huna swali?"