Jumanne , 25th Oct , 2022

Utawala wa kijeshi wa Sudan umemsimamisha kazi kamanda wa jimbo la kusini mwa nchi hiyo Blue Nile na kumteua kamanda mpya.Jeshi la nchi hiyo limetangaza hayo kupitia msemaji wake Nabil Abdallah aliyeeleza kuwa uteuzi wa kamanda mpya, ni sehemu ya juhudi za kushughulikia matukio ya kusikiti

Uamuzi huo umejiri baada ya makabiliano makali ya siku mbili ya kikabila, ambayo yamesababisha vifo vya watu 220.Mapigano ya Blue Nile karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, yalizuka upya mapema mwezi huu kufuatia mzozo wa ardhi.

Machafuko hayo yamelihusisha kabila la Hausa lenye mizizi yake Afrika Magharibi dhidi ya watu wa jamii ya Berta.Mapigano yaliongezeka Jumatano na Alhamisi wiki iliyopita katika mji wa Wad el-Mahi, karibu na mpaka wa Ethiopia.

Machafuko hayo yanafanyika mnamo wakati nchi hiyo inaelekea kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja, tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyouondoa utawala mfupi wa mpito wa kidemokrasia.