Jumatatu , 22nd Apr , 2019

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi almaarufu kama Sugu alipendekeza kurejeshwa kwa baadhi ya viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kile alichokidai kuwa viwanja hivyo vilimilikiwa wakati wa mfumo wa chama kimoja.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi

www.eatv.tv imekuletea baadhi ya vipengele ambavyo kambi hiyo ya upinzani ilivipendekeza kupiria bajeti yake kivuli ya Wizara hiyo ambapo Mbunge Sugu alishindwa kuisoma kutokana kuondolewa na baadhi ya maneno.

"Mheshimiwa Spika, kanuni za kudumu za Bunge, napenda kuwasilisha maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni  (KUB) kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, napenda kutoa pole na hongera Freeman Mbowe kwa kukaa gerezani kwa miezi 3, ameonyesha ukomavu na umahiri katika uongozi kwani kwa muda wote huo, aliendelea kukiimarisha chama, na kukifanya kuwa na mshikamano." ilisema sehemu ya bajeti hiyo ya Sugu

Sugu alieleza kuwa "siwezi kuwasahau wapiga kura wa  Mbeya, kwa jinsi wanavyonipa ushirikiano kwa hali zote, ninawashukuru zaidi hasa kwa kufunga mjadala kuhusu ubunge Mbeya Mjini, hii nawaibia siri wale wanaotaka kugombea ubunge Mbeya Mjini suala hilo lilishaamuliwa na kufungwa na wananchi wa Mbeya kwa hiyo wakajaribu kwengine"

Kuhusiana michezo

"Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka CCM kuacha mara moja kuingiza itikadi za kisiasa za chama chao  katika michezo kwani kwa kufanya hivyo inaweza kufifisha morari kwa baadhi ya wachezaji ambao si wanachama wa CCM, wala mafanikio yao hayatokani na chama wala Serikali ya CCM, bali ni juhudi zao binafsi" ameandika Sugu

Mapendekezo

Sugu amesema kuwa "viwanja vyote vya michezo vilivyopatikana na kumilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya mwaka 1992, (siasa ya vyama vingi ilipoanza), virejeshwe Serikalini, ili viweze kuendelezwa kwa ajili ya kukuza sekta ya michezo nchini."

Alhamis ya wiki iliyopita Bungeni Jijini Dodoma Mbunge huyo wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aligomea kuendelea kusoma hotuba hiyo kwa kile alichokidai kuondolewa kwa baadhi maneno ambayo aliyaandika